Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imezindua kambi maalum ya utengenezaji na urejeshaji wa mishipa ya kuchuja damu (Arterio-Venous Fistula Creation) kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo. Kambi hii inafanywa kwa ushirikiano wa wataalam wa Muhimbili-Mloganzila pamoja na jopo la madaktari kutoka Korea Kusini, ikilenga kutoa huduma bora na yenye ubora wa kimataifa.
Inatarajiwa kwamba kambi hii itakamilika tarehe 18 Februari 2026, na wagonjwa takribani 50 watapata huduma hii muhimu, ambayo itawawezesha kufanikisha matibabu yao kwa urahisi zaidi na kuboresha ubora wa maisha yao. Hii ni hatua kubwa kwa hospitali katika kuhakikisha wagonjwa wenye ugonjwa wa figo wanapata msaada wa kisayansi na wa kiteknolojia unaofaa mahitaji yao.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni