Breaking


Alhamisi, 12 Februari 2026

KIMBUNGA GEZANI CHAUWA WATU 20 MADAGASCAR


Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia huko Madagascar kufuatia Kimbunga Gezani kilichosababisha upepo mkali ulioharibu mapaa ya nyumba na kusababisha mafuriko.

Hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya kusimamia majanga katika Kisiwa cha Madagascar kilichoko Bahari Hindi.

Mamlaka hiyo imesema watu 15 hawajulikani walipo huku wengine 33 wamejeruhiwa. 

Kimbunga Gezani kilitua Madagascar, Jumanne katika mji wa pili mkubwa Toamasina, huku upepo ukipiga kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa.

Wakaazi wa mji huo wamesema upepo huo mkali umesababisha kuta za mawe kuanguka. 

Kiongozi mpya wa nchi hiyo, Kanali Michael Randrianirina, aliyechukua mamlaka mwezi Oktoba mwaka jana, ametembelea mji huo ili kujionea hali na uharibifu uliofanyika.

Hakuna maoni: