Msemaji wa kijeshi wa kundi la waasi wa M23, Willy Ngoma, ameuawa Mashariki mwa Congo.
Shirika la habari la Reuters limeripoti taarifa hizo likinukuu vyanzo vitatu vya kijeshi ikiwemo afisa mmoja wa kundi la M23.
Kulingana na vyanzo hivyo, Ngoma, ameuawa katika shambulizi la droni lililotokea eneo la Rubaya katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Siku kadhaa zilizopita, Ngoma alinusurika kuuawa katika mashambulizi kadhaa ya droni yaliyofanywa kwenye eneo hilo la vikosi vya jeshi la Congo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni