Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) imepanga kuvuka mipaka ya Tanzania na kufungua tawi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge, wakati wa ziara ya Gavana wa Jimbo la Maniema, Mussa Kabwankubi Moise, aliyeitembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Dk. Kisenge amesema JKCI inalenga kusogeza huduma za moyo kwa wananchi wa Congo, ili kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda mataifa mengine kwa matibabu maalumu.
Kwa upande wake, Gavana Kabwankubi ameeleza kuridhishwa kwake na uwekezaji mkubwa wa Serikali ya Tanzania katika JKCI, akibainisha kuwa taasisi hiyo imejipatia sifa ya kuwa kinara wa huduma bingwa za upasuaji wa moyo barani Afrika Mashariki na Kati.
Aidha, Balozi wa Tanzania nchini DRC, Juma Mshana, ameipongeza menejimenti ya JKCI kwa ushirikiano wake wa karibu na Congo, hatua inayochangia kuimarisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni