Breaking


Jumatano, 25 Februari 2026

TRUMP AFANYA HOTUBA YA HALI YA TAIFA AKIJIVUNIA “MABADILIKO MAKUBWA” MAREKENI

Rais wa Marekani, , ametoa hotuba ya Hali ya Taifa iliyokuwa na msukumo mkubwa, akijivunia kile alichokiita “mabadiliko makubwa” katika kuboresha maisha ya Wamarekani.

Hata hivyo, Trump na chama chake cha Republican wanakabiliwa na changamoto, huku kura za maoni zikionyesha kutokuwa na imani kwa Wamarekani wengi kuhusu ufanisi wake katika mwaka wake wa kwanza tangu arudi madarakani.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 79 anatumai kuwa anaweza kuwashawishi wananchi wasio na uhakika kuhusu sera zake, akisisitiza kuwa uchumi wa Marekani uko imara na una nguvu zaidi kuliko wengi wanavyodhani. Trump amesema kuwa hatua zilizofikiwa na serikali yake ndani ya mwaka mmoja ni mabadiliko yasiyo ya kawaida.

Hotuba yake inajiri wakati Marekani imepeleka manowari mbili za kivita za kubeba ndege Mashariki ya Kati, huku mvutano ukiendelea na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Hakuna maoni: