Breaking


Jumatatu, 2 Februari 2026

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KWENDA UAE KUSHIRIKI MKUTANO WA WORLD GOVERNMENT SUMMIT 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameondoka nchini leo tarehe 02 Februari, 2026 kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushiriki Mkutano wa World Government Summit (WGS) 2026 pamoja na uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS).

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo wa kimataifa unaakisi utekelezaji wa DIRA ya Taifa 2050 pamoja na Sera Mpya ya Mambo ya Nje, ambazo zimeweka diplomasia ya kiuchumi kama mhimili mkuu wa mahusiano ya kimataifa.

Kupitia jukwaa hilo, Tanzania inalenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa kuoanisha sera, kuvutia mitaji ya uwekezaji na kukuza fursa za maendeleo ya kiuchumi kwa manufaa ya taifa na wananchi wake.

Hakuna maoni: