Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 08 Februari, 2026, amezindua rasmi Soko Kuu jipya la Kariakoo lililopo Ilala, Jijini Dar es Salaam, kwa kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa soko hilo kubwa na la kisasa.
Uzinduzi wa Soko Kuu la Kariakoo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya biashara, kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira salama na ya kisasa, pamoja na kuongeza mapato ya wananchi na kukuza uchumi wa Taifa.
Katika hafla hiyo, Rais Samia aliambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakuu wa taasisi, pamoja na wageni waalikwa, ambapo walipata fursa ya kutembelea miundombinu ya soko hilo na kujionea ubora wa ujenzi pamoja na huduma zitakazotolewa.
Soko Kuu jipya la Kariakoo linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara nchini, likiwa na miundombinu inayokidhi mahitaji ya wafanyabiashara na wateja, huku likitoa ajira na fursa nyingi za kiuchumi kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.
Uzinduzi huu unaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni