Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Taifa lina imani kubwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imani ambayo imetokana na dhamana nzito waliyopewa na wananchi katika kulinda usalama na mipaka ya nchi.
Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 24, 2026, wakati wa uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT) lililopo Kikombo, mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa utii kwa mamlaka ya kikatiba pamoja na uaminifu kwa Taifa ni silaha muhimu kwa jeshi lolote linaloheshimika hivyo amelisihi Jeshi hilo kuishi kwa misingi ya viapo walivyoapa ili kulinda heshima ya Nchi na Jeshi kwa ujumla.
Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani ya nchi kwa kutumia haki zao za kikatiba, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo endelevu ya Taifa.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni