Klabu ya Yanga SC inakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) itakapokutana na AS FAR ya Morocco.
Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Gonçalves, amesema kuwa matokeo ya sare katika mchezo huo hayatakuwa mabaya kwa timu yake, huku akisisitiza kuwa ushindi utawapa uhakika wa kufuzu moja kwa moja.
“Mchezo huu ni muhimu sana kwetu. Tukishinda, tunafuzu moja kwa moja kwenda robo fainali. Tukitoa sare, bado tunaweka hai matumaini yetu,” amesema Gonçalves.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari 7, kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania, ukiwa ni miongoni mwa michezo yenye presha kubwa kwa Yanga katika msimu huu wa michuano ya kimataifa.
Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kuendelea kuisapoti timu yao kwa nguvu, wakitumaini kuona matokeo chanya yatakayoipeleka klabu hiyo hatua ya mbele zaidi barani Afrika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni