Breaking


Ijumaa, 13 Februari 2026

SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU KUKUZA HUDUMA ZA KITALII NCHINI KUPITIA MALIPO YA KIDIJITALI

 

Serikali imetangaza kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, taasisi za kifedha pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza na kuboresha huduma za kitalii nchini, hususan kupitia mifumo ya malipo ya kidijitali itakayorahisisha miamala kwa watalii wa ndani na wa kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.), jijini Arusha wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya AzamPesa kwa kushirikiana na Visa, inayolenga kurahisisha malipo ya kidijitali kwa watalii wa kimataifa wanaotembelea Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Chande amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayochochea ubunifu katika utoaji wa huduma za kitalii, akiyataka mashirika na taasisi mbalimbali kubuni njia za kisasa na salama za utoaji huduma ili kuvutia watalii zaidi na kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa taifa.

“Huduma hii italeta manufaa makubwa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uzoefu wa watalii kwa kuwapatia huduma za malipo zilizo rahisi, salama na za kisasa; kuwawezesha wafanyabiashara wa ndani; kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali; kuongeza uwazi na ufanisi katika miamala ya kifedha, sambamba na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya taifa,” alifafanua Mhe. Chande.

Huduma hiyo mpya itawawezesha watalii kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi bila hitaji la fedha taslimu, ATM au matumizi ya kadi halisi, hatua inayotarajiwa kuongeza urahisi wa biashara katika maeneo ya vivutio vya utalii, hoteli na huduma nyingine.

Mhe. Chande ameeleza kuwa ujio wa huduma hiyo umekuja wakati muafaka katika kipindi cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambapo sekta ya utalii imeendelea kuonesha ukuaji mkubwa.

Amesema kati ya mwaka 2021 hadi 2025, idadi ya watalii wa ndani imeongezeka kutoka 788,933 hadi milioni 3.6, huku watalii wa kimataifa wakiongezeka kutoka 922

Hakuna maoni: