Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ametoa maoni makali kuhusu Super Bowl Halftime Show 2026, akisema show hiyo ya rapa maarufu kutoka Puerto Rico, Bad Bunny, ilikuwa “mbaya zaidi kuwahi kutokea.”
Akizungumza na vyombo vya habari, Trump alisema kwa mujibu wake, kwa ukubwa wa Marekani, ni dharau kuona kile kilichotokea kwenye Super Bowl. Aliongeza kuwa show hiyo ilikosa ubunifu, ubora wa kisanaa, viwango vya kimataifa na uwakilishi wa mafanikio ya nchi hiyo.
Rais Trump pia alibainisha kwamba hakuelewa maneno ya nyimbo za Bad Bunny na alikosoa pia wasanii wa kucheza (dancers) waliokuwa kwenye stage, akisema walichukiza.
Hata hivyo, maoni haya yameibua mjadala mkali mtandaoni, huku mashabiki wa Bad Bunny wakidai kuwa show hiyo ilipendwa na mamilioni ya watazamaji duniani. Wengine wanasema mtazamo wa Trump ni wa kibinafsi na hauwakilishi hisia za wengi waliofurahia tamasha hilo.
Swali kwa wasomaji: Je, wewe unafikiri show ya Bad Bunny kwenye Super Bowl Halftime 2026 ilikuwa ya kufurahisha au kweli ilikuwa “mbaya zaidi”?




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni