Waziri Mkuu wa , Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo ni uthibitisho wa uongozi wa vitendo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ahadi kwa wananchi alizoahidi.
Akizungumza leo Februari 08, 2026 katika uzinduzi wa soko hilo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema ujenzi wa soko la kisasa unaonesha dhamira ya Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza usalama kwa wafanyabiashara.
Aidha ameeleza kuwa soko hilo limewekewa miundombinu muhimu ikiwemo umeme, kamera za ulinzi na jenereta za dharura, hatua itakayochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kurejesha imani ya wafanyabiashara wa Kariakoo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni