Dkt. Nchemba ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi ya fedha hizo, ambazo ni sehemu ya ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia mitaji ya mikopo nafuu.
Amesema kuwa mpango huo ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi jumuishi, kuongeza ajira na kuimarisha ustawi wa wananchi, hivyo ni wajibu wa mamlaka husika kuhakikisha fedha hizo hazipotei njiani bali zinawanufaisha walengwa halisi kama ilivyokusudiwa.
Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwawezesha vijana na wanawake ili wawe chachu ya maendeleo ya taifa na washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni