Breaking


Jumatano, 25 Februari 2026

WIZARA YA AFYA YATOA TAHADHARI KUHUSU MAFUA MAKALI, UVIKO-19, DENGUE NA KIPINDUPINDU

Serikali kupitia Wizara ya Afya  imetoa tahadhari kwa wananchi kufuatia mwenendo wa magonjwa ya mlipuko ukiwemo mafua makali ya Influenza, UVIKO-19, homa ya Dengue na Kipindupindu. 

Taarifa iliyotolewa leo Februari 25,2026 na Wizara ya Afya kupitia kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, imeeleza takwimu za ufuatiliaji zinaonesha kila mwaka katika kipindi cha mwezi Novemba hadi Aprili kunakuwa na ongezeko la ugonjwa na mafua makali ya Influenza na UVIKO-19 hapa nchini na duniani.

Aidha Wizara imesisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari binafsi ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa pale inapobidi, na kuepuka msongamano usio wa lazima.

Kuhusu Kipindupindu, Wizara imeeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana katika kudhibiti mlipuko uliokuwa umeathiri baadhi ya mikoa, bado kuna hatari ya maambukizi mapyaa hivyo wananchi wanahimizwa kuzingatia usafi wa mazingira, kunywa maji safi na salama, na kuosha matunda kabla ya kula.

Hakuna maoni: