Timu ya kikapu ya Dar City imeendelea kufanya vyema katika ligi ya mpira wa kikapu barani Afrika inayokusanya vilabu bora kutoka nchi mbalimbali kushindana kwa ubingwa wa Afrika baada ya leo kuwafunga majirani zao Nairobi City Thunder katika mchezo mkali wa kusisimua wa "Dabi Ya Afrika Mashariki" kwa jumla ya vikapu 90 huku Nairobi wao wakiwa na vikapu 85
Huu ni mchezo wa pili baada ya mchezo wa kwanza ambao walianza vyema kwa kuwafunga Johannesburg Giant vikapu 100 kwa 70.
Mchezo unaofuata Dar City watacheza dhidi ya Al Ahly Benghazi tarehe 31 ya mwezi huu wa 3.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni