Breaking


Jumatatu, 23 Machi 2026

ELIE MPANZU AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI SIMBA SC

 

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC, Elie Mpanzu kutoka DR Congo, ameongeza rasmi mkataba wake wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili zaidi, hatua iliyopokelewa kwa furaha na mashabiki wa wekundu wa Msimbazi.

 Mpanzu ambaye amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho, ataendelea kuwa sehemu muhimu ya mipango ya timu katika mashindano ya ndani na kimataifa.


Uongozi wa Simba SC umempongeza Rais wa Klabu hiyo, Mohammed Dewji, kwa juhudi zake zilizowezesha kukamilika kwa mchakato huo muhimu wa kumbakiza nyota huyo. 

Haya hiyo inaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa klabu kuimarisha kikosi chake na kuhakikisha inaendelea kuwa na ushindani mkubwa katika ligi na mashindano mengine.


Zoezi la kusaini mkataba huo limesimamiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Crescentius Magori, ambaye alisisitiza dhamira ya uongozi kuhakikisha vipaji muhimu vinabaki ndani ya timu. 

Uamuzi huo unaipa Simba SC nguvu mpya kuelekea malengo yake ya kutwaa mataji na kuendeleza mafanikio yake ndani na nje ya nchi.


Hakuna maoni: