Benki Kuu ya Tanzania (Bank of Tanzania - BoT) imetoa viwango elekezi vya ubadilishaji fedha za kigeni kwa tarehe 13 Machi 2026, vikionyesha mwenendo wa thamani ya sarafu mbalimbali dhidi ya shilingi ya Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu hizo, Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2,559.69 na kuuzwa kwa shilingi 2,585.29, huku Pauni ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 3,424.10 na kuuzwa kwa 3,458.34. Wakati huo huo, Euro (EUR) imenunuliwa kwa shilingi 2,951.07 na kuuzwa kwa 2,980.58.
Kwa upande wa sarafu za Asia, Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 372.64 na kuuzwa kwa 376.37, huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 16.09 na kuuzwa kwa 16.25. Katika ukanda wa Afrika, Rand ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 153.62 na kuuzwa kwa 155.16, wakati Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.78 na kuuzwa kwa 19.98. Sarafu nyingine ni faranga ya Rwanda (RWF), faranga ya Burundi (BIF) na shilingi ya Uganda (UGX) ambazo pia zimeonyesha viwango tofauti vya ubadilishaji katika soko la fedha.
Aidha, bei ya dhahabu katika soko hilo imeoneshwa kufikia takribani shilingi 13,229,977.6 kwa bei ya kununua na 13,362,277.38 kwa bei ya kuuza kwa kila wakia moja (Troy Ounce). BoT imeeleza kuwa viwango hivi ni vya elekezi kwa taasisi za fedha na wadau wa masoko, na hutolewa kila siku ili kusaidia shughuli za biashara, uwekezaji na ubadilishaji fedha nchini.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni