Taarifa ya viwango vya ubadilishaji fedha iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) leo Machi 31, 2026, inaonesha mwenendo wa sarafu mbalimbali za kimataifa dhidi ya shilingi ya Tanzania ukiendelea kubadilika kulingana na hali ya soko.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, dola ya Marekani imenunuliwa kwa zaidi ya shilingi 2,568, huku sarafu nyingine kama Pauni ya Uingereza na Euro zikiendelea kuwa juu zaidi, zikionesha nguvu ya sarafu hizo katika soko la fedha za kigeni.
Aidha, sarafu za nchi za Asia na Afrika kama Yuan ya China, Yen ya Japan, Rand ya Afrika Kusini pamoja na Shilingi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) nazo zimeonesha viwango tofauti vya ununuzi, hali inayodhihirisha mwingiliano wa kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa hayo.
Mabadiliko haya ya viwango vya ubadilishaji fedha huathiri moja kwa moja biashara za kimataifa, gharama za uagizaji bidhaa na hata mfumuko wa bei nchini.
Katika upande wa madini, bei ya dhahabu imefikia zaidi ya shilingi milioni 11.7 kwa wakia moja ya Troy, ikionesha kuendelea kuwa na thamani kubwa katika soko la dunia.
Ongezeko hili la bei ya dhahabu linaweza kuwa fursa kwa wachimbaji na wawekezaji wa ndani, huku pia likichochea mapato ya taifa kupitia sekta ya madini ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa Tanzania.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni