Breaking


Jumanne, 17 Machi 2026

INDICATIVE PRICES Mar. 17, 2026

 

Bei elekezi za madini zilizotolewa na Tume ya Madini leo Machi 17, 2026 zinaonesha mwenendo wa juu katika soko la kimataifa hususan kwa dhahabu, ambapo bei ya dunia imefikia dola 5,047.90 kwa wakia. 

Hali hii imepelekea pia kupanda kwa thamani ya dhahabu ndani ya soko la Tanzania, ambapo bei ya soko la madini imefikia shilingi 378,722.74 kwa gramu huku vituo vya ununuzi vikitoa hadi shilingi 370,306.68 kwa gramu. 

Ongezeko hili linaendelea kuvutia wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kutokana na faida inayotarajiwa kuongezeka.


Kwa upande wa fedha (silver), bei katika soko la dunia imefikia dola 81.27 kwa wakia, sawa na shilingi 6,774.83 kwa gramu, huku bei ya soko la ndani ikiwa shilingi 6,097.35 kwa gramu na vituo vya ununuzi vikitoa shilingi 5,961.85 kwa gramu.

 Ingawa bei ya fedha ipo chini ikilinganishwa na dhahabu, bado ina mchango muhimu katika sekta ya madini, hususan kwa wachimbaji wadogo. 

Mabadiliko haya ya bei yanaashiria umuhimu wa kufuatilia mwenendo wa soko la kimataifa, kwani huathiri moja kwa moja mapato ya wadau wa sekta ya madini nchini.


Hakuna maoni: