Joe Kent, afisa mkuu wa Trump wa kukabiliana na ugaidi ambaye alijiuzulu wiki hii kutokana na upinzani wake kwa vita nchini Iran, amezungumza na mchambuzi wa siasa za kihafidhina Tucker Carlson kwa undani zaidi kwa nini alipinga uamuzi wa Donald Trump wa kuingia vitani, ikiwa ni pamoja na ukosoaji wake wa kumshambulia Ali Khamenei.
Operesheni ya Marekani na Israel iliyomuua kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ilikuwa "jambo la mwisho ambalo tulipaswa kufanya," Kent alisema.
"Angesimamia mpango wao wa nyuklia, angewazuia kupata silaha ya nyuklia," aliongeza.
"Ukimuua kwa kumshambulia vibaya , watu wataiunga mkono serikali pamoja na Ayatollah anayekuja, na nadhani hiyo ni kweli kwa data zote tulizo nazo juu ya mtoto wake,"
Kent alisema, akimaanisha kiongozi mpya wa Iran aliyechaguliwa, Mojtaba Khamenei.
Saa moja baada ya mahojiano ya Bw. Kent na Tucker Carlson kupeperushwa, iliripotiwa kuwa FBI ilikuwa ikichunguza msimamo wa Bw. Kent.
Vyanzo kadhaa vimeiambia CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, kwamba Joe Kent, mkurugenzi wa zamani wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani, anachunguzwa na FBI.
Kulingana na CBS, uchunguzi huo unahusiana na kutolewa kwa habari za siri, na vyanzo vilisema ulianza kabla ya kujiuzulu mapema wiki hii kutokana na vita nchini Iran.
CBS ilisema FBI haikujibu ombi la maoni wakati wa kuchapishwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni