Breaking


Jumapili, 22 Machi 2026

MAKONDA ATOA MWELEKEO WA KIMKAKATI KUINUA MCHEZO WA DRIFT ARUSHA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, ametoa mwelekeo wa kimkakati wa kuendeleza mchezo wa Drift jijini Arusha, akisisitiza kuwa mchezo huo unaweza kuwa kitovu cha michezo ya magari Afrika. 

Ameeleza kuwa mafanikio ya sekta hiyo yanahitaji uwepo wa miundombinu maalum ya mashindano, mfumo wa mafunzo kwa madereva, pamoja na uwekezaji wa magari yenye viwango vya kimataifa.

Aidha, Makonda amebainisha umuhimu wa ushiriki wa vijana katika kuugeuza mchezo huo kuwa ajira na chanzo cha kipato, huku akihimiza uwepo wa wadhamini watakaosaidia kukuza sekta hiyo kiuchumi. 


Amesisitiza kuwa maendeleo ya Arusha yanapaswa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya jamii, hasa vijana, na kwamba uwekezaji katika michezo ya magari ni sehemu ya mkakati mpana wa kukuza uchumi, utalii na hadhi ya jiji kimataifa.

Hakuna maoni: