Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bloomberg, matamasha hayo mawili yalizalisha takribani dola milioni 33 za Kimarekani, sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 86.5. Inaelezwa kuwa onyesho la Ijumaa pekee lilifanikiwa kuingiza zaidi ya dola milioni 18, takribani shilingi bilioni 47.3, kupitia mauzo ya tiketi.
Takwimu hizi zinaweka matamasha hayo katika orodha ya maonyesho yenye mapato makubwa zaidi katika historia ya muziki wa moja kwa moja, zikionesha wazi nguvu ya jina na mvuto wa Kanye West kwa mashabiki wake duniani kote.
Hata hivyo, pamoja na ukubwa wa takwimu hizo, bado hazijathibitishwa rasmi na wadau huru wa tasnia ya muziki, hali inayomaanisha kuwa makadirio yanaweza kutofautiana kulingana na vyanzo mbalimbali.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni