Breaking


Jumatano, 18 Machi 2026

MALEZI YA PAMOJA YASISITIZWA KUJENGA JAMII YENYE MAADILI MEMA ZANZIBAR


Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema ili kupata maelezi bora ya jamii inatokana na malezi bora ya pamoja kwa watoto na vijana katika kujenga misingi kwenye dini tangu wakiwa wenye umri mdogo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mashindano ya Kuhifadhi Qur An yaliyofanyika Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar, Machi 18, 2026 ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Amesema ukiangalia katika jamii bado kuna mporomoko wa maadili mkubwa lakini watu wanapokutana pamoja na kuelezana basi itasaidia kujenga msingi mzuri na kuwa na jamii yenye maadili mema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Hamasi Yussuf Masauni amesema mashindano hayo yamekuwa ni mwendelezo wa miaka mingi ambapo imesaidia vijana wengi kuku ana kuwajenga kimaadili.

Masauni amesema pamoja na mambo mengine Jimbo la Kikwajuni limekuwa likisaidia Watoto wenye uhitaji mbalimbali ikiwemo katika kupata elimu.

Hakuna maoni: