Mashabiki wa Kandanda barani Ulaya wamewasilisha malalamiko kuhusu gharama kubwa ya tiketi za Kombe la Dunia la FIFA linalotarajiwa kufanyika Amerika Kaskazini msimu huu wa Joto.
Chama cha Wafuasi wa Soka Ulaya na shirika la haki za watumiaji la Euroconsumers waliwasilisha malalamiko ya kurasa 18 kwa Halmashauri Kuu ya Ulaya huko Brussels.
Kupitia taarifa ya pamoja, wamesema Shirikisho la Kandanda Duniani-FIFA linatumia udhibiti wake katika mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia la 2026 na limetumia mamlaka hayo kuweka masharti kwa mashabiki ambayo hayawezi kukubalika kamwe katika soko la ushindani"
Wanasema bei za tiketi ni kubwa zaidi kuliko mashindano yoyote yale yaliyopita ya Kombe la Dunia.
Tiketi za fainali katika Uwanja wa MetLife huko New Jersey Julai 19 zinaanzia $4,185 -ikiwa ni mara saba zaidi ya gharama ya tiketi ya bei nafuu zaidi iliyouzwa katika fainali ya Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Juni 11 mwaka huu na yatakuwa Kombe la Dunia la kwanza kushirikisha timu 48 badala ya 32.
Mashabiki watanunua tiketi kwa jumla ya mechi 104.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni