Kwa upande wa mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro na Manyara pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa na Songwe, hali ya mawingu inatarajiwa kuambatana na mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua. Aidha, kwa mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu, hali ya hewa inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
TMA imetoa angalizo kuwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Aidha, upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kaskazini mashariki kwa kasi ya takribani kilomita 30 kwa saa huku bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi. Mamlaka hiyo pia imeeleza kuwa hali ya mvua itaendelea katika maeneo mengi ya nchi hadi siku ya Jumatatu Machi 9, 2026.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni