Breaking


Jumanne, 10 Machi 2026

MHE. BALOZI OMAR ATETA NA UJUMBE KUTOKA KAMPUNI YA DANGOTE TANZANIA


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya Dangote Tanzania, ukiongozwa na Afisa Mtendaji wake Bw. Adeyemi Fajobi, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya uwekezaji katika uzalishaji wa saruji na ukuaji wa uwekezaji katika sekta ya viwanda.


Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni hiyo, Bw. Eric Kironde, Mshauri wa Kampuni hiyo, Dkt. Adelhelm Meru, Katibu wa Waziri wa Fedha, Bw. Abeid Mzee na Mchumi kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. Mustapha Muhiddin. 

Hakuna maoni: