Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila imetembelewa na wadau wake wakubwa kutoka kampuni za Humanwell Pharma Group na China Merchant Group kutoka nchini China kwa lengo la kukagua miundombinu na kubaini fursa mpya za ushirikiano katika utoaji wa huduma za afya.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ubora wa huduma za upasuaji na upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa nchini Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Godlove Mfuko, amesema ushirikiano na Humanwell Pharma Group ulianza rasmi mwaka 2024 ukilenga kusambaza vifaa muhimu vya upasuaji wa nyonga na magoti.
Kwa mujibu wa Dkt. Mfuko mchango wa kampuni hiyo umeongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma hizo kwa ufanisi zaidi na kupunguza utegemezi kutoka nje ya nchi. Huduma za upasuaji wa nyonga na magoti katika MNH-Mloganzila zilianzishwa Februari 2022, hadi sasa zaidi ya wagonjwa 400 wamenufaika na matibabu hayo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni