Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydee, amezua shauku kwa mashabiki wake baada ya kutangaza ujio wa wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachwa rasmi Machi 27, 2026.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram #ladyjaydee, Lady Jaydee aliandika:
“A new era begins on March 27th. I’ve poured my heart into this new sound, and I can’t wait for you to experience it. The countdown is officially on! Are you ready for what’s coming next?”
Akitafsiriwa kwa Kiswahili, ujumbe huo unamaanisha:
“Enzi mpya inaanza Machi 27. Nimeweka moyo wangu wote katika muziki huu mpya na siwezi kusubiri muusikie. Hesabu ya kusubiri imeanza rasmi! Je, mpo tayari kwa kinachokuja?”
Tangazo hili linakuja siku chache tu baada ya Lady Jaydee kutangazwa rasmi kama sehemu ya Universal Music Group East Africa, hatua inayotarajiwa kufungua ukurasa mpya katika safari yake ya muziki na kuipa mashabiki wake sababu zaidi ya kusherehekea.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni