Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi Machi 10, 2026 amefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa lango jipya la kuingilia watalii la Mamire lililopo upande wa magharibi mwa Hifadhi ya Taifa Tarangire, Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Ukaguzi huo ulihusisha kutembelea maendeleo ya mradi unaojumuisha ujenzi wa lango la kuingilia wageni, kisima cha maji, maegesho ya magari pamoja na mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa watalii wanaoingia hifadhini kupitia upande wa magharibi mwa Tarangire.
Dkt. Abbasi amesema kukamilika kwa mradi huo kutachochea ongezeko la watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire na kufungua zaidi fursa za kiuchumi kwa jamii zinazozunguka hifadhi hiyo.
Mradi huo ambao umefikia asilimia 98 ya utekelezaji pia unahusisha ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na uzio wa fensi katika eneo la makazi ya watumishi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni