Mwamuzi msaidizi namba moja, Kassim Mpanga, amefungiwa kwa muda wa miezi sita baada ya kukutwa na kosa la kutafsiri vibaya sheria za mchezo wakati wa dabi kali kati ya Yanga SC na Simba SC.
Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo katika dakika ya 70 ya mchezo Mpanga aliinua bendera kuashiria bao la Simba SC kuwa ni kuotea. Baada ya kupitia tukio hilo, ilibainika kuwa mchezaji aliyefunga hakuwa ameotea.
Kutokana na makosa hayo ya kiufundi katika tafsiri ya sheria, mamlaka husika zimechukua hatua ya kumfungia mwamuzi huyo kwa miezi sita.
Adhabu hiyo inalenga kudumisha viwango vya uamuzi sahihi na haki katika ligi na mashindano ya soka nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni