Waziri Mkuu, Dokta Mwigulu Nchemba, ametaka ujenzi wa jengo la huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo katika hospitali iliyopo Manispaa ya Mpanda, Waziri Mkuu, amesema Serikali imehakikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi huo.
Aidha, amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma.
Kadhalika, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watumishi bora katika sekta ya afya katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC, huku akisisitiza kuwa watumishi watakaobainika kufanya uzembe kazini watachukuliwa hatua stahiki.
Aidha, Waziri Mkuu, amesema kwa takribani miaka 60 baada ya uhuru, wilaya zote za Mkoa wa Katavi hazikuwa na hospitali za wilaya, hivyo mafanikio ya ujenzi wa hospitali mbalimbali yamepatikana katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni