Breaking


Jumatano, 8 Aprili 2026

MAFUTA YA SHUKA GHAFLA BAADA YA KUSITISHWA VITA


Bei ya mafuta duniani imepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili.

Hapo jana, Pipa moja la mafuta katika soko la kimataifa lilikuwa likiuzwa kwa dola 103.42, huku mafuta ya Marekani yakifikia takribani dola 103.25 kwa pipa. Hata hivyo, bei hizo bado ziko juu ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya mzozo kuanza Februari 28 mwaka huu.

Ichiro Kutani ni Mtaalamu wa uchumi wa nishati kutoka Japan, anasema kushuka kwa ghafla kwa bei kunahusiana moja kwa moja na tangazo hilo. 

Hata hivyo, ameonya kuwa bei huenda zisishuke hadi kufikia kiwango cha awali cha dola 70 kwa Pipa kutokana na uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati.

Nayo, masoko ya hisa barani Asia yameonesha kuimarika, ambapo Nikkei 225 ya Japan imeongezeka kwa asilimia 4 na ASX 200 ya Australia kwa asilimia 3.

Hakuna maoni: