Ndege ya kijeshi iliyokuwa na watu 121, wengi wao wanajeshi, imeanguka muda mfupi baada ya kupaa huko Puerto Leguizamo, Colombia, na kuua watu 33.
Naibu wa Meya wa Mji, Carlos Claros, amesema watu 81 walijeruhiwa katika mkasa huo.
Mji wa Puerto Leguizamo uko Putumayo, jimbo la Amazon linalopakana na Equador na Peru.
Waziri wa Ulinzi, Pedro Sánchez, amesema kwenye mtandao wa X kuwa ndege iliyoanguka Jumatatu ilikuwa ikiwasafirisha wanajeshi katika mji wa Putumayo.
Sánchez amesema hadi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa ndege hiyo ilishambuliwa na makundi ya waasi yanayoendesha harakati zao karibu na Puerto Leguizamo nchini Colombia.
Katika taarifa yake Jeshi la Anga limesema watu 77 waliokolewa kutoka eneo la ajali wakiwa na majeraha.
Msemaji kutoka Wizara ya Ulinzi alisema kwamba maafisa bado wanachunguza idadi ya mwisho ya vifo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni