Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali pamoja na kumpangia kituo Balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 18,2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, Adam Joseph Mrisho ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), na Balozi Prof. Elizabeth Kiago Kiondo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, akichukua nafasi ya Prof. Rwekaza Sympho Mukandala ambaye amemaliza muda wake.
Aidha, Balozi Noel Emmanuel Kaganda amepangiwa kituo kipya cha kazi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni