Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imepitisha Randama ya Mpango wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa Fedha 2026/2027.
Randama hiyo imewasilishwa Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), na kisha kuoitishwa na Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Thimoteo Mzava (Mb)baada ya kupitia vipaumbele vya bajeti hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa vipaumbele vilivyopo katika bajeti hiyo ikiwa ni pamoja na mpango wa kupambana na kudhibiti wanyama wakali na waharibifu, mpango wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuongeza idadi ya Watalii hadi milioni nane kufikia 2030 pamoja na sambamba na namna Wizara ilivyojipanga kuhakikisha Taifa linanufaika na michuano ya AFCON inayoandaliwa na Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda (AFCON) 2027.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Bw. Nkoba Mabula, Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo, Wakuu wa Taasisi na wataalam mbalimbali.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni