Breaking


Jumatatu, 16 Machi 2026

SERIKALI KUENDELEA KULIPA KIFUTA JASHO NA MACHOZI KWA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb.) amesema katika mwaka wa  fedha 2025/2026 Serikali imetenga shilingi 100,025,000 kwa ajili ya kifuta jasho na machozi kwa wananchi 343 wa Halmashauri ya Nsimbo waliopata madhara kutokana na changamoto ya Wanyamapori wakali na waharibifu kwenye maeneo wanayoishi


Mhe. Chande amebainisha hayo Mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), katika maeneo mbalimbali hapa nchini

Aidha, ameongeza kuwa Wizara hiyo imelipa kifuta jasho kwa wahanga 181 kwa kupitia mfumo wa Kielekroniki wa ukusanyaji wa taarifa za matukio ya Wanyamapori wakali na waharibifu (Problem Animals Information System - PAIS) huku akisisitiza waathiriwa wa matukio hayo kutumia namba za simu zilizosajiliwa kwa majina yao ili kuepuka changamoto ya mkanganyiko wa majina wakati wa malipo hali inayosababisha kuchelewa kwa malipo hayo.



"Wengine wakati wa usajili kupitia mfumo wetu wa PAIS walikua wanatumia namba za Simu ambazo zimesajiliwa kwa kutumia namba za  NIDA ambazo sio za kwao, kwenye mfumo ukitaka kutumia MUSE hayafanani Yale majina, tutahakikisha kila mhanga analipwa hata kama kwenye mfumo haijakubali tutawaelekeza watendaji wetu waje uwandani kuhakikisha kila aliyepata athari amelipwa" amesisitiza Mhe. Chande

Hakuna maoni: