Breaking


Alhamisi, 12 Machi 2026

TRA ZANZIBAR YAIPONGEZA HOTELI YA RIU PALACE KWA UADILIFU WA KODI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar tarehe 11 Machi 2026 kupitia Kaimu Meneja Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria za Kodi (Audit and Compliance), Bw. Abdallah Saleh Kombo, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Enforcement, Bw. Akiba Saaduni, wametembelea hoteli ya RIU Palace Zanzibar iliyopo Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na walipakodi pamoja na kumshukuru Meneja Mkuu wa hoteli hiyo, Bw. Hamadi Zaied, kwa kuwa miongoni mwa walipakodi wanaotekeleza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Hamadi Zaied ameishukuru TRA kwa kumtembelea na kueleza kuwa anaona fahari kulipa kodi kwani anatambua kuwa kodi huchangia maendeleo ya nchi pamoja na kuboresha huduma za kijamii. Ameahidi kuendelea kufuata sheria za kodi na kudumisha ushirikiano mzuri na TRA.

Hakuna maoni: