Breaking


Jumatano, 11 Machi 2026

UMOJA WA MATAIFA WAITAMBUA TANZANIA KUWA NCHI YENYE HISTORIA YA MUDA MREFU YA AMANI

Umoja wa Mataifa umeitambua Tanzania kuwa ni nchi yenye historia ya muda mrefu ya amani, utulivu wa kisiasa na mshikamano wa kitaifa, huku ukipongeza juhudi za nchi hiyo katika kulinda na kuimarisha amani ndani na nje ya mipaka yake.

Kauli hiyo inaonesha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa mchango wa Tanzania katika kudumisha utulivu na kuendeleza misingi ya demokrasia.

Hayo yamesemwa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Parfait Onanga-Anyanga, wakati akizungumza katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo 11 Machi 2026.

Katika mazungumzo hayo,Onanga-Anyanga alieleza kuwa Umoja wa Mataifa unatambua na kupongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha utulivu wa kisiasa, mshikamano wa kitaifa na kuendeleza misingi ya utawala wa sheria kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza kabla na wakati wa Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.

Aidha, Umoja wa Mataifa umeeleza kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania ikiwemo kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi pamoja na kuendelezwa kwa mazungumzo ya kitaifa na mchakato wa maboresho ya Katiba, hatua ambazo zinalenga kuimarisha maridhiano ya kitaifa, demokrasia na maendeleo ya kijamii nchini.

Hakuna maoni: