Serikali imesema itaendelea kuratibu na kuimarisha Sera, Sheria na Miongozo inayosimamia programu za mafunzo ya Uanagenzi na kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanagenzi nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema hayo katika chuo cha ufundi stadi Daon Bosco jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya stadi za kazi kwa njia ya Uanagenzi kwa vijana 5,746 waliodahiliwa katika vyuo 46 nchini kwa mwaka 2025/2026.
Utekelezaji wa programu umewezesha jumla ya wanufaika 93,495 hadi kufikia Februari, 2026.
Mafunzo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwapa vijana uzoefu wa kazi kwa nadharia na vitendo, kupunguza pengo la ujuzi kati ya mafunzo ya kitaaluma na mahitaji ya waajiri na kuongezeka kwa ajira kwa vijana kuajiriwa au kujiajiri.
Kwa upande wake, Naibu Katibu, Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus, amesema Serikali kupitia Ofisi hiyo, inatekeleza mafunzo ya Uanagenzi kupitia programu ya Taifa ya kukuza ujuzi nchini kuanzia mwaka 2016/17 na dhumuni la programu hiyo ni kukuza ujuzi wa nguvukazi iliyopo katika soko la ajira ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma.
Naye, Mkuu wa Chuo cha Don Bosco Dodoma, Dokta Justine Mulebya, ameshukuru Serikali kwa kukipatia chuo hicho wanafunzi 650 na ameiomba kuwawezesha vifaa wahitimu wa mafunzo ya uanagenzi ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiri vijana wengine wakihitimu mafunzo yao.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni