Breaking


Ijumaa, 17 Aprili 2026

KIFO CHA GHAFLA CHA GABBY BUGAGA CHAZUA MASWALI MAZITO BAADA YA KUKUTWA NDANI YA GARI


Kifo cha Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Vyombo vya Habari wa Burundi, Gabby Bugaga, kimeacha maswali mengi yasiyo na majibu huku taarifa za awali zikionyesha mazingira yenye utata mkubwa. 

Bugaga alikutwa amefariki dunia alfajiri ya Aprili 16, 2026, ndani ya gari katika shamba la michikichi lililopo eneo la Kivoga, kaskazini mwa jiji la Bujumbura. 

Picha zilizosambaa mitandaoni, ingawa hazijathibitishwa rasmi, zinaonyesha mtu anayedhaniwa kuwa ni kiongozi huyo akiwa ameegemea usukani wa gari aina ya Toyota Pick Up, huku gari hilo likiwa na dalili za uharibifu upande mmoja, jambo lililozua hisia kuwa huenda kulikuwa na ajali ya barabarani.


Hata hivyo, baadhi ya taarifa zimeibua utata zaidi kuhusu tukio hilo, ikiwemo ripoti kwamba mguu mmoja wa marehemu ulikuwa nje ya mlango wa gari, pamoja na madai kuwa ufunguo wa gari ulikutwa ndani ya begi badala ya kuwa kwenye gari lenyewe.

 Hali hii imezua mjadala miongoni mwa wananchi na wachambuzi, wengi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kubaini chanzo halisi cha kifo hicho. 

Licha ya sintofahamu hiyo, msemaji wa Serikali ya Burundi, Jérôme Niyonzima, amethibitisha kuwa Bugaga alifariki kutokana na ajali, huku akitoa pole kwa familia, ndugu na taifa kwa ujumla, na kumuelezea marehemu kama kiongozi jasiri aliyejitolea kulitumikia taifa lake.


Hakuna maoni: