Polisi Zanzibar wameripoti kuwa mwanamitindo anayeishi Marekani, Ashly Robinson maarufu kama Ashlee Jenae, amefariki dunia akiwa likizoni kisiwani humo na mchumba wake, Joe McCann.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Benedict Mapujira, tukio hilo lilitokea Aprili 8 baada ya wawili hao kuripotiwa kuwa na mgogoro uliosababisha kutengwa vyumba hotelini. Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini usiku huo lakini alifariki siku iliyofuata.
Hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa, huku mwili wa marehemu ukiendelea kufanyiwa uchunguzi kabla ya kusafirishwa. Tukio hilo limezua mjadala mkubwa mitandaoni, na familia yake inaendelea kushirikiana na mamlaka huku uchunguzi ukiendelea.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni