Breaking


Jumanne, 14 Aprili 2026

SIMBEYE AREJEA TPSF, APONGEZA UTENDAJI NA KUSHAURI MWELEKEO WA BAADAYE

 

TPSF imepokea kwa heshima ziara ya Godfrey Simbeye, aliyewahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo kwa takribani miaka tisa. Katika ziara hiyo, Simbeye alikutana na uongozi wa sasa unaoongozwa na Kaimu Mkurugenzi, Deogratius Massawe.


Katika mazungumzo yao, Simbeye alishiriki uzoefu wake wa kiuongozi na kutoa mapendekezo ya kimkakati kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa taifa. Alieleza kufurahishwa kwake na utendaji wa TPSF kama taasisi mwamvuli wa sekta binafsi, akipongeza juhudi za uongozi katika kusimamia ajenda za sera na utetezi kwa maslahi ya wafanyabiashara nchini.


Aidha, alisisitiza umuhimu wa uratibu mzuri wa vyama vya wafanyabiashara, akieleza kuwa ni msingi muhimu katika kuifanya Serikali kusikiliza na kushughulikia changamoto za sekta binafsi kwa ufanisi. Alibainisha kuwa juhudi zinazoendelea kufanywa na TPSF katika kuimarisha mshikamano huo zinastahili pongezi, kwani zina mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.


Kwa upande wake, TPSF imeendelea kujikita katika kuunganisha sauti ya sekta binafsi na kushirikiana kwa karibu na Serikali, ili kuhakikisha uwepo wa sera rafiki zinazochochea ukuaji wa uchumi jumuishi na endelevu.


Hakuna maoni: