Breaking


Jumatatu, 27 Aprili 2026

TRA YATOA ELIMU YA KODI KWA TAASISI YA UONGOZI WA SHULE ( TSLI)


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya kodi kwa lengo la  kuhimiza uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za kodi, pamoja na matumizi ya Mfumo Jumuishi wa Kodi za Ndani (IDRAS). Mafunzo hayo yametolewa  na Bw. Alex Mwambenja na Bi. Ajira Ismail Maafisa kutoka TRA katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Uongozi wa Shule Tanzania (TSLI).

Mkutano huo umefanyika katika Chuo cha Uongozi Mwalimu Nyerere Kibaha, ambapo washiriki walipata fursa ya kujengewa uelewa mpana kuhusu masuala ya kodi na mabadiliko yake.


Kwa upande wao, TSLI wameishukuru TRA kwa ushirikiano wao endelevu, wakieleza kuwa mafunzo yaliyotolewa yameongeza uelewa wao katika masuala ya kodi. Aidha, wameweka msisitizo wa kuendelea kufuatilia mabadiliko ya sheria za kodi kila mwaka ili kuhakikisha wanazingatia kikamilifu matakwa ya kisheria.

Hakuna maoni: