Breaking


Jumatano, 8 Aprili 2026

TRUMP ATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO KWA WIKI MBILI NCHINI IRAN


Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili dhidi ya Iran baada ya kupokea pendekezo la kumaliza vita lenye vipengele 10 kutoka Iran.

Tangazo hilo limetolewa chini ya saa mbili kabla ya tarehe ya mwisho aliyoiweka ambayo alidai kuwa ikiwa Iran haitaufungua Mlango bahari wa Hormuz basi ustaarabu mzima nchini Iran ungeangamizwa usiku wa kuamkia leo.

Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Trump amesema amefikia uamuzi huo baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif na Jenerali Asim Munir, mkuu wa jeshi mwenye nguvu nchini Pakistani.

Pakistan ambayo ni mpatanishi katika mzozo huo imethibitisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Israel pia zimekubaliana usitishaji mapigano wa haraka kila mahali, ikiwemo nchini Lebanon.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema sasa Mlango Bahari wa Hormuz utafunguliwa kwa wiki mbili, lakini kwa ushirikiano na usimamizi wa vikosi vya jeshi la Iran.

Hakuna maoni: