Inaelezwa kuwa Arsenal wanamchukulia Rogers kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, wakihitaji damu changa yenye njaa ya mafanikio. Kwa upande mwingine, Manchester United nao hawako tayari kubaki nyuma katika mbio hizo, wakiamini kuwa nyota huyo anaweza kuwa suluhisho la muda mrefu katika eneo la kiungo na kuongeza ushindani ndani ya kikosi.
Hata hivyo, bado hakuna ofa rasmi iliyowekwa hadharani kutoka kwa klabu hizo, lakini vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa mazungumzo ya awali yanaendelea kwa siri huku kila upande ukijaribu kumshawishi mchezaji huyo kuchagua mradi wao. Kadri dirisha la usajili linavyokaribia kufunguliwa, vita hii ya kumwania Rogers inatarajiwa kuwa moja ya hadithi kubwa zitakazotikisa soka la Ulaya.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni