Breaking


Jumatatu, 27 Aprili 2026

WAZIRI KOMBO ATETA NA BALOZI MKINGULE, AMHIMIZA KUIMARISHA MAHUSIANO YA TANZANIA NA CUBA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana kwa mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Cuba, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ya kidiplomasia.

Akizungumza Aprili 27, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba.

Amemtaka Balozi Mkingule kutumia vyema uzoefu alioupata alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia ili kuongeza tija katika ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa upande wake, Balozi Mkingule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba.

Aidha, amemhakikishia Waziri Kombo kuwa atafanya kazi kwa bidii kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba kwa manufaa ya pande zote mbili.

Hakuna maoni: