Katika tangazo hilo, bei ya dizeli imeongezwa kwa Shilingi 46.29 za Kenya kwa lita huku petroli ikiongezwa kwa Shilingi 16.65 kwa lita. Bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia Alhamisi Mei 15, 2026 na zitadumu kwa siku 30 zijazo.
Jijini Nairobi, petroli sasa itauzwa kwa Shilingi 214.25 za Kenya kwa lita, huku dizeli ikiuzwa kwa Shilingi 242.92 kwa lita. Mafuta ya taa yataendelea kuuzwa kwa Shilingi 152.78 za Kenya kwa lita bila mabadiliko yoyote katika kipindi hiki.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya uchumi, ongezeko hilo linaweza kuongeza gharama za usafirishaji, uzalishaji wa bidhaa na huduma nyingine muhimu, hali inayoweza kusababisha wafanyabiashara kuongeza bei kwa watumiaji wa mwisho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni