Breaking


Ijumaa, 15 Mei 2026

DP WORLD YAKAMILISHA UJENZI WA GATE 4B YA DAR ES SALAAM

Kampuni ya DP World Dar es Salaam imekamilisha ujenzi wa lango jipya la kisasa la Gate 4B pamoja na barabara ya zege ya kuingia na kutoka bandarini ikiwa ni sehemu ya maboresho makubwa ya miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Mradi huo uliotekelezwa ndani ya kipindi cha miezi 10 tangu kuanza kwa mchakato wa manunuzi hadi kukamilika kwake, unalenga kuongeza uwezo wa Bandari katika kuhudumia malori ya makontena pamoja na kupunguza msongamano wa magari bandarini.

Kupitia lango hilo jipya, uwezo wa upitishaji wa makontena umeongezeka kwa asilimia 100, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa huduma za bandari na kurahisisha shughuli za usafirishaji wa mizigo.

Aidha, Gate 4B limejengwa kwa mfumo wa kisasa wa Smart Gate wenye uwezo wa kuunganishwa na mifumo mbalimbali ya kidijitali ikiwemo vifaa vya TRA, sambamba na kuboresha mazingira ya kazi kwa maafisa wanaofanya kazi katika eneo hilo

Hakuna maoni: