Hospitali ya Taifa Muhimbili imeandaa kambi maalum ya huduma za afya mkoani Njombe itakayofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 10 Mei 2026, ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi.
Huduma zitakazotolewa ni uchunguzi wa magonjwa ya figo, uchunguzi na ushauri wa ugonjwa wa kisukari, huduma za macho pamoja na ushauri wa lishe bora.
Madaktari bingwa na wataalamu wengine wa afya kutoka hospitali hiyo wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma kwa ufanisi na viwango vya juu.
Kambi hiyo ya matibabu itafanyika katika Hoteli ya Agreement iliyopo Njombe, imelenga kuwahudumia wakazi wa mkoa huo pamoja na maeneo ya jirani, wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa ya kupata uchunguzi wa mapema, ushauri wa kitaalamu na matibabu hatua itakayosaidia kubaini na kudhibiti magonjwa kwa wakati na kuboresha afya ya jamii.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni