Breaking


Jumatano, 13 Mei 2026

MUIGIZAJI WA NIGERIA ALEX EKUBO AFARIKI DUNIA

 

Tasnia ya filamu nchini Nigeria imepata pigo kufuatia taarifa za kifo cha muigizaji maarufu wa Nollywood, Alex Ekubo, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 4O baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia wake, muigizaji huyo alifariki dunia jana, Mei 11, baada ya hali yake ya afya kuendelea kudhoofika kutokana na ugonjwa wa kansa. Familia imeeleza kuwa katika kipindi cha mwisho cha maisha yake, Alex alikuwa akipata maumivu makali yaliyotokana na ugonjwa huo.

Kifo cha Alex Ekubo kimewaacha mashabiki, waigizaji wenzake pamoja na wadau wa tasnia ya filamu barani Afrika katika majonzi makubwa. Muigizaji huyo alikuwa maarufu kwa kuigiza katika filamu mbalimbali za Nollywood na alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake cha uigizaji na mchango wake katika sanaa.

Mashabiki na watu mbalimbali wameendelea kutuma salamu za pole na rambirambi kupitia mitandao ya kijamii wakimkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani.


Hakuna maoni: